Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Sophia Simba, amesema amepokea adhabu aliyopewa na chama chake kwa moyo mkunjufu.

Bi Sophia Simba amesema hana mpango wa kujiunga na chama chochote cha siasa, kwani ataendelea kubaki kuwa mkereketwa wa chama hicho tawala.

Amesema kwa takribani miaka 46 amekuwa mwanachama mwaminifu wa CCM, hivyo haoni sababu ya kukiacha chama hicho.

Sofia ameongeza kwa kusema kuwa alijiunga na Chama cha TANU mwaka 1971, wakati huo akiwa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Katibu wa UWT Tawi la NDC nafasi ambayo alidumu nayo hadi mwaka 1979.

Baadaye mwaka 1977 alijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kuzaliwa kwake kwa hiyo hawezi kujiunga na Chama kingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *