Mwanamuziki wa miondoko ya Singeli nchini, Snura Mushi amesema anauheshimu sana wimbo wake ‘Chura’ kwa kuwa wimbo huo ndio wimbo wake wa kwanza kumtambulisha vizuri kimataifa.

Snura amesema wimbo huo umeweza kumtambulisha vizuri katika mataifa mbalimbali duniani.

Snura amesema kuwa “Nashukuru Mungu ‘Chura’ amerudi, tena vizuri, kwa sababu nilikuwa naulizwa sana kwenye majukwaa mbalimbali,”.

Pia aliongeza “Huu ndiyo wimbo wangu ulioanza kujulikana na kunitambulisha vizuri kimataifa, hivi karibuni nilikuwa na tour za kimatifa mashabiki wengi wa nje wamtaka ‘Chura’. Kwa hiyo naweza kusema wimbo wa Chura umebeba historia kubwa katika muziki wangu,”.

Video ya wimbo huo ulitangazwa kufungiwa na serikali baada ya video hiyo kukosa maadili ya kitanzania.

Kwasasa video hiyo imefunguliwa na kuanza kuchezwa katika vituo mbali mbali vya radio na Tv baada ya kufanyiwa marekebisho yaliyotakiwa na Baraza la Sanaa la Taifa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *