Mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya hip hop nchini Marekani, Snoop Dogg amejinyakulia tuzo ya heshima ya, I Am Hip-Hop kwenye utoaji wa tuzo za hip hop zilizofanyika katika ukumbi wa Cobb Energy Performing Arts Centre jijini Atlanta.

Baada ya kupokea tuzo hiyo, Snoop Dogg amewapa moyo wasanii wachanga katika kuendeleza muziki wa wa hip hop ambao ndiyo ulikuwa ukisaidia kutatua matatizo tofauti nchini Marekani.

Kwa upande mwingine Kendrick Lamar alichukua tuzo ya Lyricist of the Year kwenye tuzo hizo maarufu duniani.

Mtumbuizaji katika utoaji wa tuzo hizo alikuwa mwanamuziki wa hip hop, DJ Khaled aliyekuwa akitoa ratiba nzima ya show hiyo.

Baadhi ya wasanii walitoa burudani kwenye sherehe hizo za utaoji wa tuzo ambao ni Gucci Mane, T.I., Young Thug, Travis Scott, Desiigner na wengine kibao.

Tuzo za BET hip hop ufanyika baada ya kumalizika kwa tuzo za pamoja za BET ambapo tayari zimeshafanyika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *