Kiungo wa kimataifa wa Uholanz, Wesley Sneijder anatarajia kujiunga na klabu ya Nice inayoshiriki ligi 1 nchini Ufaransa akitokea klabu ya Galatasaray.

Klabu hiyo ya Nice imetangaza ujio wa kiuongo huyo kuwa kupitia akaunti yao ya Twitter kuwa Sneijder anatarajiwa kuwasili Ufaransa kwa ajili ya vipimo vya afya leo Jumatatu kabla ya kukamilisha usajili huo.

Miaka ya hivi karibuni Nice wamesajili wachezaji wenye majina makubwa akiwemo mshambuliaji wa Italia Mario Balotelli.

Pia wamewahi kuwasaini wachezaji kama vile Hatem Ben Arfa kutoka Newcastle, beki wa Brazil Dante na mchezaji wa Morocco Younes Belhanda miaka miwili iliyopita.

Klabu hiyo ya Nice imemaliza nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi 1 nchini Ufaransa msimu uliopita ambapo watacheza mechi ya kufuzu kombe la klabu bingwa Ulaya dhidi ya Napoli.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *