Aliyekuwa Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu amedai sakata la umri lililopelekea kuvuliwa taji la Miss Tanzania ni kitu ambacho kimebadili mfumo wa maisha yake kabisa.

Miss huyo amesema kuwa siku moja ataweka wazi ukweli kuhusu umri wake unaoleta utata miongoni mwa mashabiki wake..

Sitti ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mbunge wa Temeke Abas Mtemvu amedai kuwa sakata hilo liliweza kubadili mfumo wake mzima wa maisha kutokana na kupata coment nyingi za kumkashifu.

Mrembo huyo kwa sasa anaendelea kufanya bishara ya kitabu chache cha Chozi la Sitti ambacho alikiandika baada ya sakata hilo.

Sitti amesema kitabu hicho kitaweza kuwasaidia vijana wengi hasa wakike katika nyanja mbalimbali za maisha.

Sitti Mtevu alivuliwa taji la miss Tanzania mwaka 2014 baada ya kujulikana ana umri mkubwa kuliko aliotajwa ikiwa ni kosa kwenye mashindano hayo ya urembo nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *