Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro amesema kuwa atahakikisha mauaji ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji yanamaliziki kabisa.

Kamanda Sirro amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwaza toka ateuliwe kuwa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini akichukua nafasi ya Erenest Mangu.

Sirro amesema kuwa atahakikisha wakazi wa Rufiji wanaishi kwa amani kama ilivyokuwa apo awali kabla ya mauaji ya viongozi kuuawa ndani ya wilaya hizo mkoani Pwani.

kamanda Sirro amewataka wananchi kumuunga mkono kwenye kazi yake hiyo ili kuhakikisha uhalifu unapungua nchini.

Pia Kamanda Sirro ameahidi zawadi ya shilingi milioni 10 kwa mtu yoyote atakayetoa taarifa sahihi kuhusu wauaji wa Kibiti waliouwa viongozi wa vijiji na Vitongoji.

Kwa upande mwingine IGP, Sirro amewataka madereva wa bodaboda na kuwataka kuacha kuvunja sheria za barabarani kwa makusudi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *