Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro amewataka Watanzania wawe wavumilivu kwa kuwa Polisi wanafanya uchunguzi wa kina kuhusu mauaji yanayoendelea mkoani Pwani.

Sirro ameyasema hayo jana katika ziara yake ya kwanza mkoani Morogoro tangu ateuliwe kuwa IGP na kusisitiza kuwa polisi wanafanya kazi usiku kucha kudumisha hali ya usalama.

Pia amesema kuwa “Hatulali, tunafanya kazi kwa juhudi kubwa, lakini ni lazima wananchi watupe ushirikiano na nyinyi waandishi wa habari pia mnatakiwa mwandike kwa hekima bila uchochezi’.

Sirro amesema amefanya ziara hiyo Morogoro na katika maeneo mengine nchini ili kuzungumza na polisi namna ya  kusimamia ulinzi na usalama katika maeneo yao.

IGP Sirro alifanya ziara mkoani Pwani maeneo ya Kibiti kwa jaii ya kufanya mazungumzo na waakazi wa maeneo hayo ili kupata chanzo cha matukio hayo ya mauji watu yanayoendelea ndani ya mkoa wa Pwani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *