Kamanda wa polisi mkoa wa Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa kama mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ana wasi wasi na jeshi la polisi kuhusu kudhibiti matumizi ya shisha achukue hauta zaidi kwasababu yeye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.

Kamanda Sirro amesema wao kama jeshi la polisi wanafanyakazi kwa mujibu wa sheria na operesheni ya kutokomeza shisha yanaendelea kama kawaida kilichobaki ni mwanasheria mkuu kuwafungulia mashitaka watuhumiwa.

Kauli hiyo ya Kamanda Sirro imekuja baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kusema kuwa uhenda kamanda Sirro ameongwa na wamiliki wa shisha jijini Dar es Salaam na ndiyo mana wameshindwa kuzuia zoezi hilo.

Juzi waziri  Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema atamwajibisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda iwapo hatasimamia ipasavyo kukomesha matumizi ya shisha.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *