Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Sirro amesema kuwa kukosekana kwa ushahidi pamoja na gharama kubwa za kuwatunza wahalifu ndio sababu zinazofanya wahalifu wengi kuachiwa wanapokafikishwa kituoni.

Sirro amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kutoa ushahidi wa kesi wanazofungua ili watu wahalifu hao wafungwe kwa mujibu wa sheria badala ya kulaumu jeshi la polisi.

Amesema kitendo cha wananchi kukwepa kujitokeza kutoa ushahidi wa kuwatia watu hatiani kunaiongezea gharama kubwa jeshi hilo kwa ajili ya kuwatunza, kuwahifadhi na kuwahudumia kwa chakula.

Pia amesema Watanzania wengi wamekuwa na tabia ya kulaumu jeshi la polisi pale wanapomuona mtuhumiwa aliyekamatwa na vidhibiti akiwa ameachiwa huru pasipo kujua kuwa kesi yoyote lazima itolewe ushahidi ndipo mtuhumiwa aweze kufungwa kwa mujibu wa sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *