Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amewataka watu wote waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuhusika na dawa za kulevya, kuripoti kituo kikuu cha polisi kama walivyoamrishwa.

Kamanda Sirro amesema leo ndiyo siku ambayo walitakiwa kuripoti kituoni hapo, lakini hadi majira ya saa 7 mchana walikuwa ni watu wanne pekee ambao walikuwa wamekwisha ripoti tofauti na wale wawili walioripoti jana.

Kwa upande mwingine Sirro amesema kuwa Manji na Gwajima ambao wameripoti jana wanaendelea kushikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi juu ya kuhusishwa na dawa za kulevya.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliwataja watu 65 wanahojiusisha na madawa ya kulevya ambao walitakiwa kuripoti kituo cha Polisi kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo ambazo zinawahusu.

Washukiwa hao waliotakiwa kuripoti leo ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Mmiliki wa Cyclif pamoja mmiliki wa maduka ya Hussein Pamba Kali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *