Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema jeshi la polisi haliwezi kuua raia asiye na hatia.

Sirro ameyasema hayo leo kwa wanahabari alipozungumzia mauaji ya kijana mmoja kwenye mashine ya kutolea pesa (ATM) ya CRDB Bank eneo la  Kurasini jijini Dar es Salaam  ambapo baadhi ya ndugu wa marehemu wanadai hakuwa jambazi kama polisi wanavyodai.

Hayo yamejiri baada kuenea kwa taarifa kuwa kijana aliyeuwa na Polisi maeneo ya Kurasini jijini Dar es Salaam hakuwa jambazi kama Polisi wanavyoripoti.

“Naomba niwaeleze watu wa mitandao ya kijamii inayosema kuwa polisi wameua kijana ambaye ni mtumishi wa Mungu na mwanachuo. Ukweli ni kwamba ndugu wanaweza kuona kijana wao anatoka nyumbani kwenda shuleni, kumbe ana mambo yake.

Kwa upande miwingine Kamanda Sirro amewatahadharisha wananchi kuhusu wizi mpya ulioibuka ambapo amesema  mtuhumiwa mmoja, Dunia Hamisi (36) mkazi wa Mikocheni jijini Dar es Salaam alikamatwa kwa madai ya kupora watembea kwa miguu kwa kutumia gari lenye usajili namba T 732 BAZ aina ya Toyota Cresta GX100.

Amesema mtuhumiwa anayehojiwa atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika ambapo tayari amewataja wengine anaoshirikiana nao katika uporaji huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *