Kamanda Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP), Simon Sirro ametoa agizo kuwa mchakato ufanyike wa kuzivunja timu zote za jeshi la polisi zinazoshiriki ligi za soka za madaraja tofauti ili iundwe timu moja.

Kamanda Sirro amesema kuwa hatua hiyo itachukuliwa ili kuifanya timu moja ambayo itaundwa iwe na nguvu na kuwe na maandalizi mazuri kuliko ilivyo sasa ambapo kuna timu nyingi lakini hazifanyi vizuri.

IGP Sirro amesema amesisitiza kuwa ameshatoa mwongozo kwa kamishna wa idara husika ili mchakato wa kuzifuta timu zilizopo katika madaraja tofauti ufanyike kwa faida ya kulipa jeshi nguvu liwe na timu moja imara.

 Timu hiyo ambayo itaundwa itafahamika kwa jina kla Polisi Tanzania na itakuwa inachukua wachezaji wenye vipaji vya juu kutoka katika vituo mbalimbali vya jeshi la polisi.

Kuhusu michezo mingine, IGP Sirro amesema inafanyika lakini vijana wake wanahitaji motisha ili waweze kuonekana, na kusisitiza kuwa hilo litafanyika ili kuboresha michezo mingine ikiwemo ndondi, mieleka na judo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *