Waziri wa nchi ofisi ya rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene ameitaka mikoa saba ambayo imeshindwa kutekeleza agizo la kuwa na madawati ya kutosha kufanikisha zoezi hilo ifikapo Januari mwakani.

Waziri huyo amewataka wakuu wa mikoa na wilaya hawajatimiza kuhakikisha wanafanikisha mpango huo ifikapo Januari 2017 na kama hawatafanya hivyo atawashitaki kwa Rais.

Simbachawene amesema hayo alipokuwa anapokea madawati 3,550 kutoka benki ya NMB yaliyotengenezwa na kampuni ya ndani ya EDOSAMA, waziri huyo amesema kuwa anamashaka na utendaji wa wakuu wa mikoa hao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa NMB, Ineke Bassemaker amesema kuwa waliaidi kutoa madawadi na sasa wanaona ni fahari kubwa kwao na kufanya hivyo ni kuboresha elimu ya Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *