Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene amewataka wakuu wa wilaya wastaafu ambao hawakuteuliwa katika kipindi cha awamu ya tano, kutosikitika na kukata tamaa kwa kukosa nafasi hiyo badala yake waitumie fursa waliyonayo kujiendeleza zaidi.
Simbachawene pia amewahakikishia viongozi hao waliomaliza muda wao kuwa kwa mujibu wa Rais John Magufuli, mchakato wa mafao yao tayari umeanza kutekelezwa na muda wowote wataanza kulipwa mafao hayo.

Akifungua semina ya mafunzo ya ujasiriamali iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kwa wakuu hao wa wilaya pamoja na viongozi wengine wastaafu.

Waziri huyo amesema ni jambo la kawaida kila uongozi mpya unapoingia madarakani kubadilisha timu yake ya kufanyia kazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *