Klabu ya Simba imeingia rasmi kambini kujiandaa kwa ajili ya mchezo wa ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya watani wao wa jadi Yanga SC siku ya Jumamosi Oktoba mosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo wa mzunguko wa saba wa ligi hiyo unatarajiwa kupigwa siku ya Jumamosi Oktoba Mosi mwaka huu, katika dimba la Taifa Dar es Salaam, ambapo Simba imepania kulipa kisasi cha kufungwa na Yanga katika michezo yote miwili ya msimu uliopita wa ligi hiyo.

Meneja wa klabu hiyo Musa Hassan amesema maandalizi ya kuchukua point tatu katika mchezo huo yameanza na kwamba tayari timu imeingia kambini ikiwa chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na kocha Joseph Omog pamoja na msaidizi wake Jackson Mayanja.

Hata hivyo, Mgosi amekataa kuweka wazi mahali ambapo kambi ya wekundu hao wa Msimbazi imewekwa bila kutaja sababu yoyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *