Klabu ya Simba imeitangaza Kamati Maalum itakayohusika na kumtafuta mzabuni ambaye atanunua hisa 50% za timu hiyo katika suala lake la uendeshaji mpya wa klabu hiyo.

Kamati hiyo itaundwa na wajumbe wa 5 na itaongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo pamoja na wajumbe wa 4 ambao ni Wakili Damas Ndumbaro, Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu, Yussuf Majjid Nassor na Abdulrazak Badru ambaye ni Mkurugenzi wa Bodi ua Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania.

Kamati itakutana Alhamisi September 6 mwaka huu kuanza kazi ya kuwajadili wanachama ambao watataka kuzinunua hisa hizo ambapo watafuata sheria za manunuzi ya umma ambapo watakaa kwasiku 45 kabla ya kumtangaza mzabuni wa timu hiyo.

Kamati hiyo ambayo itakuwa huru itafanya kazi zake kwa kuzingatia taratibu zote za kimanunuzi kwa mujibu wa sharia na taratibu za nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *