Klabu ya soka ya Simba imetozwa faini ya shilingi 5,000,000 (milioni tano) pamoja na kulipa gharama za uharibifu wa viti uliofanywa na mashabiki wa klabu hiyo.

Bodi ya Ligi ya shirikisho la soka nchini TFF  imesema kwamba maamuzi hayo yamefikiwa leo katika kikao cha Kamati ya Masaa 72 ya shirikisho hilo.

Adhabu hiyo imetokana baada ya mashabiki wa Simba kung’oa viti wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Yanga uliochewa Oktoba Mosi kwenye uwanja wa taifa.

Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetoa adhabu kwa vilabu kadhaa kufutia vilabu hivyo kukutwa na makosa mbalimbali.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *