Simba inatarajia kumsajili golikipa wa klabu ya Medeama ya Ghana, Daniel Agyei kwa ajili ya kuichezea timu hiyo kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania bara itakayoanza mapema mwezi huu.

Msemaji wa Simba, Haji Manara, alisema ujio wa kipa huyo ni ishara ya kuelekea kuwa mabingwa wa Tanzania Bara, msimu huu kama walivyokusudia mwanzoni mwa msimu.

Mchezaji huyo ameletwa nchini kutokana na repoti ya kocha wao Joseph Omog, raia wa Cameroon, kuuagiza uongozi kutafuta kipa mwingine ambaye atampa chalenji Vicenti Agban ambaye amedaka peke yake mechi zote za mzunguko wa kwanza.

Amesema kutua kwa Agyei haimaanishi kuwa watamtupia virago Agban, bali wataendelea kuwa naye pamoja na kinda Manyika Peter, ili kuongeza ushindani wa kuwania nafasi ya kucheza wenyewe kwa wenyewe.

Agyei anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao wa zamani wa Tanzania na uwezekano wa kipa huyo kushindwana na Simba ni mdogo, kwani tayari ameutaka uongozi wake wasimjumuishe kwenye mipango yao ya msimu ujao.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *