Simba imekanusha taarifa za kutaka kuliondoa benchi lake la ufundi chini ya kocha Joseph Omog na msaidizi wake Mganda Jackson Mayanja.

Hayo yamesemwa leo na afisa habari wa klabu hiyo Haji Manara ambapo amesema taarifa zozote zinazoenezwa si za kweli na klabu inaendelea na benchi lake kama kawaida.

Manara amesema kuwa “Kuhusu makocha Simba bado inaendelea na benchi lake la ufundi chini ya mwalimu Omog na Mayanja hakuna mabadiliko yoyote yaliyofanyika”.

Aidha Manara amesema kikosi cha Simba kinaingia kambini leo kuanza maandalizi ya mchezo wao wa ligi kuu wikiendi ijayo dhidi ya Njombe Mji kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.

Pia Manara amempongeza Mwenyekiti mpya wa Bodi ya ligi TPLB ambaye pia ni Katibu wa Yanga Clement Sanga ambapo amesema klabu ya Simba itampa ushirkiano ili kutatua changamoto zilizopo kwenye ligi kuu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *