Timu za vijana za Simba na Azam FC zinatarajia kucheza kwenye mchezo wa fainali ya Ligi Kuu ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 utakaochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Timu hizo zilifuzu hatua hiyo juzi ambapo Azam FC waliifunga Mtibwa Sugar kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya kumaliza dakika 120 bila kufungana na Simba ilikata tiketi ya fainali kwa kuifunga Stand United mikwaju ya penalti 8-7 baada ya kumaliza dakika 120 kwa sare ya bao 1-1.

Azam imefuzu fainali hizo kutoka kituo cha Kagera na Simba ilikuwa kituo cha Dar es Salaam na ndio zilikuwa zikiongoza kwenye vituo vyao.

Hii ni mara ya kwanza kwa ligi hiyo ya vijana kuchezwa nchini. Ligi hiyo imedhaminiwa na Azam na Diamond Bank.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *