Klabu ya Simba inatarajia kufanya mkutano wa wanachama wa dharura utakaofanyika Desemba 11 mwaka huu.

Mkutano huo umeitishwa baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji wa klabu hiyo iliyokaa juzi na kuamua mkutano huo.

Ofisa habari wa klabu hiyo, Haji Manara amesema kuwa mkutano huo utafanyika kwenye ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Amesema Kamati ya Utendaji imetoa baraka zake kupitia ibara ya 22 ya Katiba ya Simba.

Pia amesema kuwa mkutano huo utakuwa ni mwendelezo wa mkutano wa kawaida uliofanyika Julai 31 mwaka huu.

Hata hivyo, taarifa hiyo haijaeleza ajenda za mkutano huo, lakini inadaiwa kuwa huenda ukahusu kuboresha suala la uongozi wa Simba na kuingia katika suala la uwekezaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *