Simba SC inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Polisi Dodoma siku ya Ijumaa kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Afisa habari wa klabu hiyo, Haji Manara amesema kwamba mechi hiyo imetokana na maombi ya Chama cha soka Dodoma ambao wameiomba klabu hiyo kwenda kucheza mechi ya kirafiki ili kuinua molali ya soka mkoani humo.

Tiimu hiyo anatarajia kuondoka leo kuelekea Dodoma tayari kwa ajili ya mechi hiyo ya kirafiki.

Haji Manara: Afisa habari wa klabu ya Simba SC.
Haji Manara: Afisa habari wa klabu ya Simba SC.

Manara ameongeza kwa kusema kwamba kutokana na michezo ya ligi kusimama kutokana na timu ya taifa ambayo inawachezaji sita kutoka Simba wameona ni vyema kulifanyia kazi ombi la wakazi wa Dodoma.

Pia amesema mechi hiyo itakuwa ni sehemu ya maandalizi kwa kocha Joseph Omog kuelekea kwenye mechi yao ijayo ya ligi kuu Tanzania Bara.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *