Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga amewaomba viongozi wa dini kuiunga mkono mamlaka hiyo.

Sianga amewataka viongozi wa dini kutoa mchango wao kwa sababu inafanya kazi kubwa ambayo inahitaji msaada wa watu wote.

Kamishna Sianga amesema hayo jana katika ufunguzi wa kongamano kuhusu mmomonyoko wa maadili na athari za dawa za kulevya lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).

Pia BAKWATA wameshirikiana na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, lililofanyika mjini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu, Kassim majaliwa amewaomba viongozi wa dini nchini kutumia nafasi zao kuhimiza wazazi na walezi kuishi maisha yenye nidhamu.

Pia amesema kuwa inabidi viongozi wa duni kuhimiza wazazi hao kuthamini kazi yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu na kusimamia malezi ya watoto na kuzingatia maadili ya Taifa kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *