Muigizaji na mchekeshaji maarufu wa Bongo Movie, Steven Mangere (Steve Nyerere) anatarajia kufanya show yake ya uchekeshaji jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi.

Steve Nyerere amesema show hiyo ameipa jina la ‘East African STANDUP COMEDY’ inatarajiwa kufanyika katika Hotel ya Protea iliyopo jijini Dar es Salaam siku ya jumamosi ya wiki hii.

Mwigizaji huyo amewataka watanzania kuhudhuria katika show hiyo kwani itakuwa na mambo tofauti katika uchekshaji na watafurahi pindi watakapojitokeza kwenye show hiyo.

Steve Nyerere amejizolea sifa katika tasnia ya movie hapa nchini baada ya kushiriki katika movie tofauti.

Mbali na uigizaji Steve Nyerere pia ana kipaji cha kuigiza sauti za viongozi mbali mbali hapa nchini ambapo alikuwa anaigiza sauti ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na ndiyo mana hadi sasa anajulikana kama Steve Nyerere.

Katika hatua nyingine Steve Nyerere amesema kwamba yeye ni mmoja wa mastaa wanaomiliki nyumba nyingi hapa nchini lakini hapendi kuzionesha kwa kuwa yeye si mtu wa kupenda sifa kama walivyo mastaa wengine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *