Mwanamuziki  wa Singeli, Sholo Mwamba amemchana  msanii mwenzake, Man Fongo kuwa ameridhika kwa muda mfupi baada ya kuachia nyimbo ya ‘Hainaga Ushemeji’  wakati kazi ndiyo kwanza inaanza.

Sholo Mwamba anayetikisha na Ngoma ya Sembe Tembele amesema kuwa Man Fongo alikuwa DJ wake na hata mwanzoni alikuwa akitumia jina la Man Fongo Mwamba.

Mwanamuziki huyo amesema “Zamani Man Fongo alikuwa DJ wangu, kipindi napata shoo za mkoa nilikuwa nikimuachia kitengo ambapo kama sipo walikuwa wakimuita Man Fongo Mwamba”.

Man Fongo
Man Fongo

Sholo Mwamba aliendelea kusema “Ukaribu ukaenda sana, nimekuwa naye kwenye maisha magumu yote tatizo lake alipotoa ngoma ya Hainaga Ushemeji anaona tayari kamaliza kila kitu wakati safari bado ndefu”.

Pia aliongeza kwa kusema “Ukisikiliza hapa kati baada ya Hainaga Ushemeji ametoka wimbo wa Kibaka na mwingine lakini zote bado hazijafikia ubora wa Hainaga ushemeji hapo utaona kwa jinsi gani alivyobweteka kuishi na ngoma moja na kushindwa kufanya ngoma kali kuzidi ya kwanza,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *