Shirikisho kubwa na lenye nguvu zaidi la wafanyakazi nchini Afrika Kusini, Cosatu, limemtaka rais Jacob Zuma kung’oka madarakani.

Katibu mkuu wa shirikisho hilo, Bheki Ntshalintshali ametangaza kuwa rais Zuma ‘sio mtu sahihi’ wa kuiongoz anchi hiyo.

Shinikizo za kumtaka ajiuzuru wadhifa wa uraisi sambamba na wadhifa wa Uenyekiti wa chama cha ANC zimezidi kuongezeka kwa rais Zuma kufuatia mabadiliko ya baraza la mawaziri ambayo yalijumuisha kumfuta kazi aliyekuwa waziri wa fedha, Pravin Gordhan ambaye anaaminiwa na wengi.

Tangu kufanywa kwa mabadiliko ya baraza hilo la mawaziri thamani ya Randi ya nchi hiyo imeendelea kushuka kwa kasi na kutishia ustawi wa uchumi wan chi hiyo ambao tayari umetetereka.

Cosatu, ambalo ni sehemu muhimu ya utawala wan chi hiyo ina jumla ya wanachama 1.8m.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *