Shirika la ndege Marekani la Delta limetangaza kusitisha na kuchelewesha safari zake baada ya kutokea matatizo ya mfumo wa komputa wa ndege zake kote duniani.

Delta imesitisha tena safari baada ya kukatisha safari zake siku ya jumatatu na kuwaacha maelfu ya wasafiri wakihangaika.

Baadhi ya abiria waliokwama na ndege hiyo.
Baadhi ya abiria waliokwama na ndege hiyo.

kushindwa kwa mfumo wa komputa wa kampuni hiyo ulisababishwa na kukatika kwa umeme katika makao mkuu mjini Atlanta.

Shirika hilo la Delta limesema kuwa abiria waliositishiwa safari au kucheleweshwa watapewa ndege nyingine au kurudishiwa gharama zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *