Mkali wa Bongo Fleva, Shilole amekanusha kuvuruga ndoa ya aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Nuh Mziwanda.

Shilole amesema kuwa hakurudiana na Nuh kama habari zinavyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuonekana wakiwa pamoja jijinini Mwanza.

Kupitia mitandao ya kijamii zilizagaa taarifa kwamba wawili hao wamerudia na wako karibu zaidi.

Shilole amedai kwa sasa yeye na Nuh ni washikaji na kuna baadhi ya show wanaandaa pamoja ndio maana kuna wakati wanaonekana wako pamoja lakini hawapo kwenye mahusiano kama inavyodaiwa.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa “Mimi na Nuh sasa hivi ni washikaji, hatuwezi kugombana kama zamani, mimi na Nuh tumesaidiana vitu vingi sana kwa hiyo bado kunaushikaji fulani. Pia sisi ni wasanii, mkituona pamoja mjue kuna kazi zinaendelea, mnajua Nuh ana mke kwahiyo hayo mambo sio ya kweli, kwanza navunjaje ndoa yao?,” .

Mbali na hilo Shilole amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kwajili ya kazi mpya zinazotarajiwa kutoka hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *