Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed maarufu kwa jina la Shilole amesema kuwa anatarajia kufunga ndoa mwezi Disemba mwaka huu.

Shilole amesema kuwa anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake wa sasa Ashraf Uchebe ifikapo Disemba 20 mwaka huu ambapo ndiyo itakuwa siku yake ya kuzaliwa.

Mwanamuziki huyo ameamua kuweka wazi siku yake ya ndoa baada ya kuibuka utata kufuatia akaunti moja ya Instagram inayosomeka jina la Uchebe kuandika maneno ya kumkejeli mwanamuziki huyo.

Kufuatia akaunti hiyo kuandika habari hiyo, Shilole amesema kuwa akaunti hiyo ya Instagram siyo ya mpenzi wake huyo bali imetengezwa na baadhi ya watu ili kumuaribia mahusiano yake ya mpenzi wake huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *