Staa wa Bongo fleva, Shilole amemtetea Bill Nass kwa kusema kwamba hana tatizo na mtu pia ni kijana mtulivu sana.

Staa huyo ameongea hayo baada ya TID kudai kuwa Bill Nas hana shukrani kutokana na kumsadia kufanikiwa kimuziki ambapo alikuwa chini ya kampuni ya Rada Entertainment inayomilikiwa na TID.

TID
TID

Shilole amesema watu wanamuonea sana Bill Nas kwasababu  ni kijana mtulivu ambaye anaelewa nini anafanya kwenye kazi yake kwani hapendi competition ila kuna watu wanataka kufanya competition naye na kutaka kutengeneza jambo ambalo halina maana.

Pia Shilole ameongeza kwa kusema ni kweli hakuna mtu aliyemjua Bill Nas kabla hajawa kwa TID lakini anaamini anamheshimu sana Bosi wake huyo wa zamani.

Bill Nas kwasasa anamilikiwa na kampuni ya ‘LFLG’ inayosimamia kazi zake zote za kimuziki baada ya kutoka kwa TID.

Bill Nas
Bill Nas

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *