Mkali wa muziki wa Bongo fleva, Shilole ameamua kujikita katika kazi ya mama lishe na kuanza kuuza chakula kwa staili ya kuwapelekea wateja wake walipo.

Shilole amesema kuwa biashara hiyo anaamini itakuwa na wateja wengi na itamwingizia kipato tofauti na mastaa wengine ambao wamekuwa waking’ang’ania biashara zisizokuwa na tija ilimradi waonekane tu.

Mkai\li huyo amesema kuwa “Mimi nafanya biashara ambayo nina uhakika nayo ya kupata wateja na baada ya muda nitajua faida ninayoipata, mimi napambana kujenga maisha yangu.

Mwanamuziki huyo licha ya umaarufu mkubwa lakini amekuwa akijichanganya kushiriki masuala mbalimbali ya kibiashara huku mwenyewe akidai kwamba staili hiyo ndiyo itakayomfanya anufaike na ustaa wake badala ya kukaa ndani na kuwa tegemezi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *