Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amekanusha taarifa kuwa kushindwa kuachia ngoma kwa kipindi cha miezi mitano ni kutokana na kudukuliwa kwa mtandao wake wa (Instagram).

Shilole amesema kuwa watu wanaozungumza kwamba yeye amekaa kimya muda mrefu ni kutokana na wengi wao kumiss kuona vituko na tashtiti zake katika mitandao ya kijamii hivyo hata wakati akiwa amejiandaa kutoa wimbo mpya bado alionekana kama kapooza.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa “Siyo kweli kama nategemea Instagram kutoa kazi, kwani bila hiyo Insta zamani watu walikuwa wanafanyaje? Sijatoa wimbo kwa sababu nilitaka wimbo wa ‘hatutoi kiki uendelee kusogea na siyo kwamba kwa sababu nilikuwa sina mtandao wa Instagram ndiyo nikaamua nitulie.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa Lakini kwa sababu najua kuna wasiosikiliza radio na na wasiotazama Tv ndiyo maana pia nilitulia kuusoma mchezo kwa kuwa nilitaka niwapate wote na mashabiki mashabiki wa mtandaoni ndiyo maana nilichelewa kidogo”.

Shilole ameongeza kuwa “mashabiki waliopokea wimbo wangu huu ndiyo mashabiki wa kweli siyo wale wanaosubiri tashititi za kukaa uchi au kelele zangu ila.

Akizungumzia kuhusu mahusiano yake msanii Shilole amekanusha taarifa zinazoenea mitandaoni kuwa mume wake mtarajiwa ndiye mwanaume anayeonekana katika video yake mpya ya ‘Kigori’.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *