Staa wa Bongo fleva, Shetta kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa mwezi ujao wa Ramadhan amejotolea kutoa misaada kwa vituo vya watoto yatima.

Sheta amesema hayo kufuatia kubaki wiki chache tu kabla ya kuingia katika mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Kupitia ukurasa wake wa instagram, Shetta ameandika kuwa “Msimu wa Ramadhan unakaribia Mimi kama Shetta na menejimenti Yangu nzima napenda kukufahamisha kuwa kwa kidogo nilichonacho natarajia kuanza kusaidia na kutoa misaada kwa vituo vya watoto yatima na wenye uhitaji mkubwa mikoa yote ya Tanzania ambayo Ntaweza kuifikia.

Pia ameongeza kwa kusema kuwa Naamini Vipo vituo vingi vyenye uhitaji mkubwa sana wa mahitaji ya kila siku.Hivyo basi popote ulipo kama unajua au unahusika na kituo chochote usisite kuwasiliana nasi kupitia;

Social media( Instagram, Tiwtter, FaceBook; @OfficialShetta or @MxCarter )
Email; shettamusic@gmail.com or MxCarter@slidevisuals.com
Simu; +255 22 278 0288 / 0655653030.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *