Kampuni kubwa ya teknolojia ya Google imewawaita wafanyakazi wake waliokuwa safarini nje ya Marekani kurejea haraka nchini humo kufuatia rais Trump kusaini sheria ya kuwazuia raia kutoka nchi 7 duniani kutoingia Marekani.

 Google imewaita wafanyakazi wake wanaofikia 100 ambao wanatoka kwenye mataifa yaliyotajwa na Trump kutoruhusiwa kuingia Marekani.

Hata hivyo hatua hiyo ya rais Trump imeendelea kuzua mgongano wa mawazo huku makampuni mengi ya teknolojia yanayotegemea wataalamu kutoka nje ya Marekani ikiwemo kampuni ya Microsoft ikiwaonya wawekezaji wake kuwa sheria hiyo inaweza kuathiri biashara zao.

Wataalamu wa teknolojia kutoka nje ya Marekani ambao pamoja na kulipwa vizuri pia hupewa viza maalum aina ya H1-B kwaajili ya kuishi Marekani.

Sheria mpya iliyosainiwa na rais Trump imekataa kutoa viza kwa raia kutoka nchi saba za kiislamu huku viza kwa raia wa Iran na Iraq zikizuiwa kwa kipindi cha miezi mitatu.

Nchi zilizozuiwa kuingiza raia wake nchini Marekani ni Iran, Iraq, Syria, Yemen, Sudan, Somalia na Libya ambapo hata kama raia wake watakuwa wanakwenda nchi nyingine kwa ndege zinazopitia Marekani, hawataruhusiwa kupanda ndege hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *