Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohamed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufungaji wa kampeni wa uchaguzi mdogo katika jimbo la Dimani Mjini Unguja kesho.

Kiongozi mwingine atakayehudhuria ufungaji wa kampeni hiyo ni Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wengine wa Chama hicho tawala.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Idara kamati maalumu ya NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Zanzibar Waride Bakar Jab wakati akiongea na wanahabari kuhusu ufungwaji wa kampeni za chama hicho.

Pia amesema kuwa matarajio ya chama hicho ni kuendeleza historia ya ushindi katika jimbo hilo la Dimani mjini Unguja.

Uchaguzi mdogo wa jimbo la Dimani unafanyika kufutokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wake, Hafidh Ali Tahir (CCM) kilichotokea Novemba 11 mkoani Dodoma alikokuwa akihudhuria Mkutano wa Bunge na kuugua ghafla.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *