Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein, leo anatarajia kukiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalumu ya NEC Zanzibar – Idara ya Itikadi na Uenezi, Waride Bakar Jabu, kikao hicho cha kawaida cha siku moja kitafanyika Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui kuanzia saa 4 asubuhi.

Amesema kuwa kikao pamoja na mambo mengine, kitapokea na kujadili Mapendekezo ya wanachama wa CCM wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Dimani na kuongeza kuwa maandalizi yote yamekamilika.

Pia Katibu Waride amesema kikao hicho kilitanguliwa na Kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC, chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, kwa lengo la kuandaa ajenda za kikao hicho.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *