Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda leo ameripoti Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam ‘Central’ kama alivyotakiwa kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa.

Sheikh Ponda amesindikizwa na jopo la wanasheria wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti CHADEMA Bara, Prof. Abdallah Safari na kwenda moja kwa moja kwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa, jana alimpa siku 3 tu Sheikh Ponda, ili kujisalimisha na kuhojiwa kuhusu tuhuma zinazomkabili, na iwapo hatafanya hivyo watamchukulia sheria stahiki.

Juzi, Jeshi hilo lilivamia mkutano wa Sheikh Ponda aliokuwa nafanya na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, na kufanikiwa kukamata baadhi ya watu wakiwemo waandishi wa habari ambao walikuwepo kwenye mkutano huo.

.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *