Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum amesema jitihada zinazofanywa na Rais John Magufuli za kulinda rasilimali za taifa zinaenda sawa na mafundisho ya dini ya kiislamu.

Alhad ameyasema hayo leo wakati akitoa hutuba baada ya swala ya Eid El Fitr katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Amesema katika mafundisho ya dini ya kiislamu kuchezea rasilimali ni haramu, hivyo Waislamu na Watanzania kwa ujumla wanapaswa kuunga mkono jitihada hizo za kulinda rasilimali za taifa.

Amesema kuwa “Jitihada anazofanya Rais wetu ni sawa kabisa na mafundisho ya dini yetu ya Kiislamu, anachofanya ni kulinda keki ya taifa ili kila mmoja anufaike na keki hiyo, hili ni jambo zuri,”.

Pia amewataka waislamu kuitumia sikukuu ya leo kuliombea taifa amani na kuwaombea viongozi wote ili waweze kutekeleza yaliyo mema kwa ajili ya Watanzania wote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *