Staa wa Bongo movie, Shamsa Ford amesema ataendelea kuwa mwanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) licha ya uchaguzi mkuu kumalizika mwaka jana.

Staa huyo amesema kwamba Edward Lowassa bado ana nafasi kwake na ni kumbukumbu ya maisha yake na siku zote atakuwa na nafasi moyoni mwake kwa sababu ndiye kiongozi aliyemchagua na bado ataendelea kumheshimu.

Shamsa Ford: Akiwa na wasanii wenzake, Aunty Ezekiel na Jacqueline Wolper katika mkutano wa CHADEMA mwaka jana.Shamsa Ford: Akiwa na wasanii wenzake, Aunty Ezekiel na Jacqueline Wolper katika mkutano wa CHADEMA mwaka jana.

Shamsa Ford ameyasema hayo baada ya muigizaji mwenzake, Jacqueline Wolper kutangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wiki iliyopita kwenye mkutano wa kumchagua mwenyekiti mpya wa chama hicho uliofanyika mkoani Dodoma.

Shamsa Ford, Aunty Ezekiel na Jacqueline Wolper walikuwa bega kwa bega na aliyekuwa mgombea urais anayeungwa na vyama vinavyounda umoja wa UKAWA, Edward Lowasa katika kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana ambapo Rais John Pombe Magufuli ameibuka na ushindi.

Jacqueline Wolper: Akitangaza kurejea CCM katika mkutano uliofanyika Dodoma. Jacqueline Wolper: Akitangaza kurejea CCM katika mkutano uliofanyika Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *