Staa wa Bongo movie, Shamsa Ford ameamua kuweka wazi mahusiano yake baada ya kumtambulisha mpenzi wake katika sherehe ya siku yake ya kuzaliwa ambapo hapo awali alikuwa akimficha.

Shamsa amesema kwamba baada ya kutendwa mara kadhaa na wanaume wake wa hapo awali alikuwa anaogopa kuweka wazi mahusiano yake lakini sasa ameamua kuweka wazi kwasababu anamuamini mpenzi wake huyo.

Staa huyo amesema anakuwaga mzito labda kwa sababu ya uwoga lakini mapenzi yakikuzidi mwisho wa siku unashindwa kujizuia ni kweli ametolewa mahari.

Pia Shamsa akusita kumwagia sifa mama yake mzazi huku akimshukuru kwa malezi mazuri ambayo yamemfanya aonekane mtu mbele ya watu na kumfanya apate heshima popote aendapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *