Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amefunguka na kuwapa somo mastaa wenzake wasichague wanaume wa kufunga nao ndoa kwa kusubiri matajiri.

Shamsa Ford amewaambia mastaa haokukumbuka kuwa hata hao matajiri wana watu wao huku wakisahau kuwa ndoa ni baraka toka kwa Mungu.

Shamsa amefunguka hayo huku akiendelea kuwakumbusha wasanii kwamba, waache tabia za kuchagua wanaume wa kuwaoa kwani leo wana majina makubwa na wanaonekana warembo lakini ipo siku itafika hata hao wanaume wanaowatongoza leo watapotea kabisa.

“Ndoa ni ngumu usipomuweka Mungu mbele, usipokuwa mvumilivu,usipoziba masikio, usipokuwa na imani. wasichana wenzangu maisha ni mafupi sana leo tunavuma na kupendwa kila kona tunapokatiza ila kuna muda utafika hata nzi hakusogelei.Hata uwe mzuri na maarufu kiasi gani lakini ndoa ina heshima yake” -Shamsa Ford.

Aidha Shamsa ameongeza kwamba “Msiwe wachaguzi sana, maana ukisema unamsubili tajiri aje akuoe na yeye huyo tajiri ana mwanamke wake aliyetoka naye mbali kimaisha, Cha muhimu ni kumuomba Mungu akupe mwanaume mwenye kumjua Mungu, upendo, heshima, mtafutaji hayo mengine yanakuja tu. Nguvu ya mmoja ni tofauti na ya wawili”-

Muigizaji huo kwasasa ameolewa na mfanyabiashara wa nguo nchini Chid Mapenzi ambaye anamiliki baadhi ya maduka ya nguo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *