Shamsa Ford awafungukia wanaosema amemfilisi mumewe

0
359

Baada ya kuenea habari katika mitandao ya kijamii kuwa muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amemfilisi mumewe Chid Mapenzi, muigizaji huyo amewajia juu na kuwajibu watu hao.

Kupitia akaunti yake ya Instagram mkali huyo ameandika maneno makali kwa ajili ya watu hao wanaotaka kumualibia ndoa yake.

Muigizaji huyo ameanza kwa kusema kuwa ‘Nikiwa kama binadamu ni vibaya kuishi na kinyongo kwasababu natembea na umauti na sijui ni lini Mungu atanichukua’.

Ameendelea ‘kiukweli mmenisononesha sana binadamu..ila kubwa kuliko vyote nimegundua kwamba watu wengi hawaitakii ndoa yangu mema’.

Pia ameongeza kwa kusema ‘Nilipoanzana uhusiano na mume wangu wakasema tutachezeana na kuachana.Tulipooana wakasema hatutofikisha mwezi tutaachana, mitihani mingi iliyotutokea binadamu hawahawa walikuwa wanacheka’.

Ameendelea kwa kusema ‘Leo hii mnatusimanga na hayo mambo mnayopost..Nyie Binadamu mnataka nini jamani..Ni wa kwangu Mimi hata aweje ni wa kwangu mimi.Mnalotaka litutokee inshaallah kwa kudra za Mwenyezi Mungu halitatokea’.

Mwisho amemalizia kwa kusema kuwa ‘Pale mnapowaza mabaya yatutokee kwenye maisha yetu na Mungu naye anapanga kutuepusha na hayo mabalaa’.

LEAVE A REPLY