Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amewachana vibaya wanaume wanaopenda kulelewa na wanawake maarufu kama ‘Marioo’.

Kupitia mtandao wa Instagram muigizaji huyo ameonyeshwa kukasirishwa na tabia hiyo ambayo inapelekea wawe tegemezi kwa wapenzi hao kutokana na kuchagua kazi za kufanya hususani hapa Dar es Salaam.

Shamsa ameanza kwa kuandika “Kaka zangu na wadogo zangu wa kiume ningependa kuwashauli mpende kujituma na kufanya kazi kwa bidii, usitamani kazi ya kuzunguka kwenye kiti ofisini wakati elimu yako ni darasa la pili. Mwanaume unatakiwa ujitume na kupambana na maisha, sukuma hata mkokoteni ilimradi ujipatie riziki.,”.

Pia ameongeza kwa kuandika  “Sasa nyie kaka zangu wa sasa hivi yaani hampendi kufanya kazi ukishajiona una sura nzuri basi na wewe eti unadanga kwa jimama lenye pesa.

Mwisho amemaliza kwa kuandika “Sasa kama mwanamke anakufuga wewe unadhani atakuheshimu?utachezea kuchapwa vibao na kutukanwa, hivi hamuumii na haya majina mnayoitwa?mara vibenten,vipanyabuku,vichura,vitom and jerry…daah.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *