Muigizaji nyota wa Bongo movie, Shamsa Ford amewashauri wanawake wenzake kuachana na kutumia vitu feki ili waonekane warembo.

Katika ukurasa wake wa instagram Shamsa amepost video ikimuonesha binti akicheza muziki club na kuangukwa na magodoro aliyoyaweka kwenye makalio, kisha kuandika ujumbe mzito akiwaasa wanawake kujiamini na kukubali uumbaji wa Mungu.

 

Katika video hiyo Shamsa ameandika kuwa “Wanawake wenzangu hebu tujiamini jamani na tuuamini uumbaji wa Mungu, Mungu ana sababu ya kukuumba hivyo ulivyo, kama wewe ni mweusi baki na weusi wako, kama huna shape kama mimi baki hivyo hivyo, maana wengine ndo wanachoma masindano ya kuongeza makalio au hips, mwisho wa siku unapata cancer”.

 

Muingizaji amesema kuwa yeye binafsi anajikubali na ana amini Mungu ana kila sababu ya kumuumba hivyo alivyo hivyo hata ukimsema vibaya kwa jinsi alivyo hajali.

Muigizaji huyo amejizolea umaarufu kupitia filamu zake tofauti alizoigiza hapa nchini akiwa na baadhi ya mastaa wenzake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *