Shamsa Ford atamani kuolewa tena

0
49

Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amesema kwa sasa yupo tayari kuolewa kwa mara nyingine baada ya ndoa yake ya awali kuvunjika.

Shamsa aliweka picha yake na kusindikiza na ujumbe huo ya kwamba yupo tayari kuolewa.

“Tangu nimetoka kwenye ndoa ni miaka 3 sasa. Nimejipa muda wa kutosha na kupata elimu kubwa juu ya mahusiano. Sasa hivi akili yangu imetulia nipo tayari kuolewa tena inshaaallah.

“Sitaki kuendelea kufanya zinaa mimi ni binadamu sijui mwisho wangu ni upi. Inshaaallah Mwenyezi Mungu unipe mume mwenye kheri na mimi atayenipenda, kunithamini na kunitunza.Mume atayempenda mwanangu na atayesimama kuwa baba bora kwa mwanangu maana kila ninapokwenda nipo naye.”

Shamsa alifunga ndoa mfanyabiashara Rashidi Said ‘Chidi Mapenzi’ mwaka 2016 na kisha ndoa yao kuvunjika baadaye.

LEAVE A REPLY