Muigizaji nyota wa Bongo movie, Shamsa Ford amesema kuwa amepokea maswali mengi kutoka kwa mashabiki wake wakimuuliza kama ni kweli ameacha kuigiza baada ya kuolewa.

Shamsa Ford amesema kwamba hawezi kuacha movie kama mashabiki wanavyomuuliza na kusisitiza kuwa uigizaji ndiyo kazi yake na hawezi kuiacha.

Muigizaji huyo ambaye alifunga ndoa mwezi mmoja na nusu uliopita na mfanyabishara wa maduka ya nguo, Chidi Mapenzi amesema ndoa haiwezi kumtenganisha na mashabiki wake wa filamu.

Shamsa amesema kuwa kwasasa anategemea kuachia movie zake mbili ‘Chale Mvuvi’ na ‘Dhamana’ kwa mashabiki wake wakae mkao wa kuzipokea movie hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *