Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amefunguka kuwa na kusema kuwa kuna mwanamke anamletea figisu figusu dhidi ya mume wake.

Shamsa Ford Muigizaji huyo amesema hayo kwa madai kuna mwanamke anamletea figisu figisu mume wake  anayefahamika kama Chid Mapenzi.

Kupitia akaunti yake Instagram “Nakupenda mume wangu halali wa ndoa aliyenipa mwenyezi Mungu. Sitoachana na wewe kwa ajili ya makelele ya wanadamu nitaachana na wewe kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Unanipenda, unaniheshimu, unajishusha kuomba msamaha pale unapokosea wakati wanaume wengine hawawezi kuomba msamaha hata wakikosea”.

Pia ameongeza kwa kuandika “Mume wangu nikikuelewa Mimi inatosha wengine wakipiga kelele tuchukulie kama burudani tu. Maana anajitahidi huyo anayeitwa ILALA MJINGA kama ulivyomsave kwenye simu yako kusambaza msg kwenye magroup na kuwatumia waandishi ushahidi. Jamani sitokuja kumuacha mume wangu kwa ajili ya mwanamke hata siku moja labda afanye makubwa yasiyoeleweka kwenye jamiii. Amecheat Bili clinton sembuse Rashid wangu ? Nakupenda RASHID WA SHAMSA FORD tupambane tuzidi kujenga familia yetu.”

Muigizaji huyo ameandika hayo baada ya kutokea kwa taarifa za kuwepo kwa mwanamke kuingilia ndoa yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *