Muigizaji wa Bongo Movie, Shamsa Ford amejitaja kuwa mwanamke wa nguvu kwenye biashara huku akitaja kuwa alianza na biashara ya kuunga unga kwa kuibia kuuza ndani ya duka la aliyekuwa mume wake hadi sasa anamiliki lake.

Lakini wakati anapambana msanii huyo aliwahi kuingia hasara kwani aliibiwa mzigo baada ya dereva bodaboda na bajaji aliowatuma kumchukulia mzigo wa Sh12 milioni kupata ajali na watu kuiba baadhi ya mzigo eneo la tukio.

Muigizaji huyo alisema duka la aliyekuwa mume wake Chid Mapenzi lilikuwa linauza nguo za kiume huku akijaribu kuuza nguo za kike aina ya vijora alianza na vitambaa vitano ambavyo vimempa duka sasa.

“Vitano nilipata wateja wengi ambao walikuwa wananishawishi kuendelea kuwatafutia ili niwauzie baada ya ndoa kuvunjika niliendeleza biashara yangu ambayo ilinibeba kutokana na uaminifu nilianza na mkopo wa 500,000,” alisema na kuongeza;

“Hadi sasa namiliki duka ambalo pamoja na mafanikio niliwahi kupata hasara lakini haikunikatisha tamaa kwani ni biashara ambayo naipenda na naifurahia kuifanya.”

Shamsa alisema aliagiza mzigo baada ya kufika aliwatuma boda boda wawili na bajaji mbili wamfuatie ulikuwa na thamani ya Sh 12 milioni.

“Huwezi kuamini nilipata hasara kubwa sana kwani boda walipata ajali hivyo kukatokea wizi eneo la tukio niliambulia mzigo wa Sh 3 milioni kupitia shida hiyo nilijifunza kitu ambacho kimenisaidia kuongeza umakini,” alisema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *