Muigizaji nyota wa Bongo movie, Shamsa Ford amefunga ndoa na Rashidi Said ‘Chidi Mapenzi’ ambaye ni mfanyabiashara wa maduka ya nguo hapa nchini.

Sherehe za ndoa hiyo zimefanyika nyumbani kwa wazazi wa Shamsa eneo la Sinza, Afrikasana jijini Dar es Salaam.

Hapo awali Shamsa alidumu katika penzi na Dickson Matoke ‘Dick’ na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume aitwaye Terry na kisha  kufunga ndoa ya kimila nyumbani kwa mwanaume huyo, Tarime mkoani Mara.

Baada e wawili hao waliachana na kuangukia kwa staa wa Bongo Fleva Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ambaye penzi lao halikudumu.

Shamsa Ford ameamua kuolewa na mwanaume kama walivyofanya baadhi ya waigizaji wenzake wa Bongo Movie kama Flora Mvungi ambaye amefunga ndoa na mwanamuziki wa Bongo Fleva, H- Baba ambapo hadi sasa wamefanikiwa kupata watoto wawili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *