Madaktari na watoa misaada nchini Syria, wameituhumu helikopta moja inayopdaiwa kudondosha mapipa yaliyokuwa na gesi ya sumu ya krolaini kwenye mji wa kaskazini mwa Syria.

Takribani watu 30 wametaarifiwa kuathirika na shambulizi hilo ambalo limetokea kwenye mji wa Saraqeb kwenye jimbo la Idlib.

Pande zote zinazoshirki kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo zimetuhumiana juu ya shambulio hilo huku kila upande ukikanusha kuhusika na shambulizi hilo.

Dkt. Abdel Aziz Bareeh, anayefanya kazi kwenye mji wa Saraqeb, ameliambia shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC, kuwa mapipa hayo ya gesi ya krolaini yalidondoshwa Jumatatu jioni.

‘Tunatambua kuwa hii ni krolaini kwakuwa tulishawahi kushambuliwa nayo kipindi cha nyuma hivyo tunaifahamu harufu yake na dalili zake….tuna wagonjwa 28 waliothibitika kuathirika na gesi hii wengi wao ni kina mama na watoto’

Shirika la wafanyakazi wa uokozi wa kujitolea limesema linahisi kuwa hilo ni shambulio la krolaini lakini limeshindwa kuthibitisha.

Krolaini ni kemikali inayotumika viwandani lakini matumizi yake kwenye silaha yamepigwa marufuku katika mkataba wa kimataifa wa matumiki ya kemikali za sumu.

Dalili kubwa za shambulio la sumu ya krolaini ni pamoja na macho kuuma, ngozi kuwasha na kuuma, kushindwa kupumua na kutoka damu mdomoni’.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *